Kituo cha Rasilimali

Kituo cha Rasilimali

🪟 Je, ungependa usionwe kabisa na wengine unapokuwa ndani ya intaneti?

Soma hapa:

Kwa kawaida, huwa unaacha nyayo nyingi za taarifa unapoingia mtandaoni. Hata hivyo, kuna ujanja unaoweza kuutumia, “joho la kujificha ” uwapo ndani ya intaneti. Hili huitwa VPN, ambacho ni kifupi cha “Virtual Private Network”. Unapotumia VPN, unatuma data zako zote kupitia handaki lisiloweza kuingiwa na mtu mwingine yeyote.

Ili kufanya hivi, unapaswa kusakinisha programu ya VPN kwenye kifaa chako. Jambo hili hupendekezwa sana, kwa mfano, pale unapotumia mtandao wa WiFi unaotolewa bure au wa umma, usio na ulinzi wowote.

Usakinishi na utumizi wa VPN unaweza usiwe jambo rahisi.

Ndani ya baadhi ya nchi, kufanya hivi kunaweza kuwa kinyume cha sheria.

Hivyo basi, ni vema ukafanya kwanza utafiti na ukalinganisha chaguzi zilizopo, ama muombe mtu mzima (wazazi, walimu au wengineo) akusaidie na kukujulisha kuhusu sheria zilizopo ndani ya nchi yako.

Programu “nzuri” na “mbaya” za kiroboti (bots), zina tofauti gani?

‘Bots’ ni programu za kompyuta zinazotenda kazi kana kwamba ni binadamu. Programu hizi hutengenezwa na wataalamu wa kompyuta ili ziweze kufanya kazi fulani.

‘Bots’ zinaweza kufanya kazi hizi upesi zaidi kuliko binadamu. Baadhi ya programu “nzuri” za kiroboti hufanya kazi zinazotusaidia kama watumizi, kama vile

  • 🤖 Programu za kiroboti za kutoa huduma kwa wateja, ambazo huzungumza nasi kupitia jumbe za maandishi ili kutatua tatizo fulani upesi na hivyo kutuondolea adha ya kusubiri mida mirefu kupita kiasi.

Programu nyingine za kiroboti husababisha matatizo kwani hutengenezwa kwa madhumuni ya kutekeleza shughuli za kudhuru na hata zinazokiuka sheria.

Mifano baadhi hii hapa:

  • 🤖 – Programu za kiroboti za kitapeli zinazokusanya anuani za barua pepe, data binafsi au taarifa nyingine za mtumizi ili kutuma jumbe kibao za kitapeli (barua pepe na matangazo yasiyohitajika)
  • 🤖 Programu za kiroboti za kijamii ni wasifu wa mitandao ya kijamii zilizotengenezwa kiautomatiki na ambazo kisha hupakia picha, hutuma jumbe, au kusambaza maoni fulani kiautomatiki ndani ya mtandao wa kijamii- kwa mfano, kupitia onyesho la mapendo, maoni, au njia ya ushirikishaji.
  • 🤖 Programu za kiroboti za kijamii zinaweza kusababisha matatizo makubwa pale zinaposambaza taarifa nyingi za uongo, zinapotumika kuwanyanyasa watumizi wengine wa mtandao huo husika wa kijamii, na zinapochochea chuki. Itasaidia kama, utazuia wasifu husika wa programu ya kiroboti na kisha kuuripoti.

Je, umewahi kutakiwa kutatua fumbo fulani la kihesabu ama kuchagua picha zote zinazoonyesha umbo la gari wakati unapotengeneza akaunti mpya ya mtandao wa kijamii ama pindi unapojisajili kwenye tukio fulani mtandaoni?

Hizi ni njia zinazotumika kuzuia programu za kiroboti za kitapeli ili zisiweze kukusanya taarifa zako binafsi na anuani yako ya barua pepe.

Vidakuzi Mtandaoni? 🍪🍪🍪Je, tunaweza kuvitafuna? Havihusiani kabisa na biskuti tunazozifahamu (kwa bahati mbaya).

Hebu tutizame tofauti iliyopo baina ya vidakuzi vizuri na vibaya:

Bila shaka umewahi kusikia kuhusu vidakuzi… Ni “chembechembe” ndogo unazoziacha baada ya kumaliza kutumia intaneti, ili tovuti husika ulizozitembelea ziweze kukutambua wakati mwingine. Jambo hili linaweza kuwa jema, kwa mfano, ukicheza mchezo fulani na kisha kuweza kuanzia kutoka kwenye alama yako ya awali pindi utakaporejea kucheza mchezo huo.

Lakini pia, jambo hili linaweza kuwa si jema, kwani tovuti hizi zinaweza kutaka kukutumia matangazo ama kushirikisha taarifa zako kwa madhumuni mengineyo.

Unaweza kuepuka vidakuzi kwa kuvinjari intaneti ukiwa ndani ya mandhari binafsi🕵️‍♂️. Kupata mandhari haya binafsi, bonyeza upande wa kulia wa kipanya cha kompyuta yako, juu ya ishara ya kivinjari chako (k.m. Google Chrome au Internet explorer) ili kufungua menyu iliyopo, na kisha chagua dirisha jipya binafsi.

Je, una fahamu kuwa unaweza kulinda simujanja 📱 yako kwa kutumia kifunga skrini?

1) Android
⚙️Mipangilio ➡️ Ulinzi ➡️ Kifunga skrini na kisha bonyeza aina ya kifunga skrini kama vile PIN

2) iPhone
⚙️Mipangilio ➡️ Mwonekano na Mwanga ➡️ Kifunga skrini cha kiautomatiki na kisha chagua muda (k.m. baada ya sekunde 30)

Ikiwa kama kompyuta 💻 yako inatumiwa pia na watu wengine, unaweza kutengeneza akaunti ya mgeni kwa ajili ya hao watu wengine.

Fuata hatua hizi rahisi:

Kama unatumia kompyuta inayoendeshwa na mfumo wa Windows, bonyeza alama ya ‘Start’ iliyopo upande wa chini mkono wa kushoto. Nenda kwenye ⚙️Mipangilio ➡️Akaunti na kisha bonyeza “Familia & watumizi wengine” ama “barua pepe na akaunti”.

Kisha, chagua chaguzi la “Ongeza Akaunti”, na kisha chagua “Ongeza mtumizi asiye na akaunti ya Microsoft”. Baada ya hapo unaweza kuingiza jina la mtumizi na nywila ya akaunti hiyo ya mgeni.

Kutengeneza akaunti ya mgeni katika MacBook yako, bonyeza alama ya ‘Apple’ iliyopo upande wa juu kona ya kushoto na kisha chagua kipengele cha menyu cha “Watumizi na makundi” kilichopo kwenye mipangilio ya mfumo.

Orodha ya Vitu vya Kukagua: Namna ya kutambua taarifa ya uongo 🤨

Je, umewahi kukutana na jambo la kustaajabisha kwelikweli ndani ya intaneti, jambo lililokufanya ufikiri: “Hili haliwezi kuwa kweli? Ni la kustaajabisha sana kwangu!”
Unaonaje – je, kila mara unaweza kuziamini taarifa zilizopo kwenye intaneti? Ikiwa hauna uhakika, tizama orodha ifuatayo. Endapo kama kipengele chochote ndani ya orodha hii kitahusika kwenye taarifa hiyo, basi jua ya kwamba taarifa hiyo inaweza kuwa taarifa ya uongo.

✅ Je, ni tovuti yenye mwonekano wa ajabu ama wa kimasihara?
✅ Je, umewahi kusikia lolote kuhusu mwandishi wa taarifa hiyo?
✅ Je, picha na maneno yanafanana, au je kuna kitu kinachoonekana kuleta ukakasi katika picha hiyo?
✅ Je, kuna idadi kubwa sana ya makosa katika maandishi hayo, kwa mfano kwenye barua pepe?
✅ Je, simulizi hiyo ni ya zamani na haihusiani kabisa na mambo yanayotokea sasa?
✅ Je, kiungo hicho kimekusudiwa kubofya ama je, kinachochea hisia fulani?
✅ Je, kuna jambo lolote linaloonekana kuwa na utata kwako?

🛍️ Huenda na wewe umeliona hili pia: Matangazo yaliyopo kwenye intaneti yanaweza kukera sana. Hata hivyo, lipo jambo unaloweza kufanya …

Vizuizi vizuri vya matangazo husaidia kuhakikisha kwamba huonyeshwi tena matangazo ya aina fulani. Hata hivyo, havitoi ulinzi wa asilimia 100 kwani havina uwezo wa kuchuja kila kitu. Baadhi ya vizuizi vizuri vya matangazo ni uBlock Origin ama Google Chrome Ad Blocker.

Rasilimali za Nyongeza:

Hapa unaweza kupata taarifa zaidi kuhusiana na programu za kiroboti (bots):

Nambari za simu ya kitaifa ya usaidizi kwa maswala ya watoto: https://childhelplineinternational.org/helplines/

Kwa Kiingereza (na Vidakuzi):