Nyumbani

Welcome to the Digital Enquirer Kit Youth!

Are you ready to make the internet a safer space for you and your friends? Then start your learning journey now, become a Digital Enquirer and gather the tools for your personal Enquirer Kit!

Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer) ni nani?

Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer) ni mtu anayefahamu namna ya kutambua taarifa za uongo na namna ya kutafuta, kuchambua, kuhakiki, na kushirikisha kwa usalama taarifa za kuaminika mtandaoni. Na kiujumla, neno ‘Mdadisi’ humaanisha nini? Ni mtu anayeuliza maswali, anayetaka kujifunza zaidi, na anayetafakari kwa kina kuhusu hatua anazozichukua.

Utajifunza nini?

Ndani ya kozi hii, utaweza kuwa Mdadisi wa Kidigitali (Digital Enquirer) makini na utajifunza namna ya kujilinda na namna ya kuvilinda vifaa vyako. Pia, utajifunza:

  • Namna ya kushughulikia taarifa zilizopo kwenye ulimwengu wa kidigitali
  • Namna ya kutambua taarifa za uongo na namna ya kuzishughulikia
  • Namna ya kuwalinda marafiki yako, familia, na wengineo

Inachukua muda kiasi gani kukamilisha kozi hii?

Kiasi cha muda kinachohitajika kukamilisha kozi hutofautiana baina ya mtu na mtu. Kozi hii imegawanywa katika masomo manane na masomo haya yamegawanywa katika sura kadhaa. Hivyo, unaweza kuingia kwenye sura mpya ndani ya dakika chache tu. Hata hivyo, kwa kuwa hatutumii vidakuzi kutokana na kutotaka kukusanya data zako, hautaweza kuhifadhi mtiririko wa historia ya maendeleo yako.

Endapo kama utaanza kusoma somo fulani lakini ukahisi kushindwa kukamilisha sura zote, baadae utakaporejea kwenye somo hilo, utaweza kuruka kwenda moja kwa moja kwenye sura uliyokomea kwa kutumia menyu iliyopo ndani ya somo hilo.

Turtle atafurahi kukuona tena! 🐢

Information for caregiver and teachers

Pamoja na Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali ya Vijana (DEK Youth), kuna mwongozo ulioandaliwa kwa ajili ya walimu. Kupitia mwongozo huu, tunataka kuwasaidia walimu, wazazi, wakufunzi, na walezi wengine katika kutumia kozi ya Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali kwa Vijana (DEK Youth) wawapo darasani, wawapo na familia zao, ama katika klabu za kundi za vijana. Kwa kuwa kozi ya Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali ya Vijana (DEK Youth) imewalenga vijana wenye umri unaozidi miaka 10, tumekusudia kutokukusanya data zozote. Hili linamaanisha kwamba, kwa mfano, hakutakuwa na vidakuzi vyovyote vitakavyotumika kwenye kozi hii. Watu wazima pamoja na vijana, ambao wangependa kujifunza mengi zaidi baada ya kukamilisha kozi hii, wanaalikwa kutembelea kozi ya Nyenzo ya Mdadisi wa Kidigitali (DEK) inayopatikana kwenye jukwaa la atingi.

Kozi hii imeandaliwa kwa ajili ya nani?

Kozi ya Mdadisi wa Kidigitali ya Vijana (DEK Youth course) imelenga watoto na vijana wenye umri unaozidi miaka 10.